Information in Swahili
2014
Aina mpya ya uyogategemezi unaoharibu mazao na mimiea mikoa ya kusini mwa Tanzani
Mikoa ya kusini mwa Tanzania imekumbwa na janga la aina mpya ya uyogategemezi unaoshambulia mazao na miti aina mbalimbali. Mradi wa ushirikiano wa utafiti kati ya Chuokikuu cha Dar es Salaam na Chuokikuu cha Uppsala nchini Swedeni, unalenga juu ya kuutambua uyoga huo, namna unavyoshambulia na kuua mimea pamoja na kuungana na jitihada zingine nchini kupendekeza namna ya kuutokomeza ugonjwa huo. Uyoga huu hushambulia miti ya aina zote yaani miti pori na ile iliyopandwa kwa kuifanya ikauke ndani ya muda usiozidi myezi mitatu tangu kuonekana kwa dalili zake. Mazao kama vile mihogo, nanasi pia hushambuliwa na kuoza. Mpaka sasa uyoga huo imeishajulikana kuwa upo katika jamii ya ‘Polyporales’ yaani uyoga wenye matundu mengi. Utafiti unaendelea kwa kutumia njia za ulinganifu wa muonekano na vinasaba ili kutambua aina yake halisi kisayansi. Mradi huu unadhaminiwa na shirika la utafiti la kiswidi ‘ Swedish Research Link’ kwa ajili ya kudumisha ushirikiano wa tafiti za pamoja na mahusiano ya kitaaluma katika nchi hizi mbili.
2015
Warsha yenye mafanikio: 27/7 - 1/8 ilifanyika warsha ya kimataifa juu ya 'Systematic and Omics in Biology' katika idara ya IOB. Washiriki saba kutoka Tanzania, walimu nane kutoka idara ya ‘Systematic biology’ na mmoja kutoka idara ya ‘Museum of Evolution’ wamechangia katika warsha hiyo nzuri na yenye mazingira mazuri ya kijamii. Warsha hiyo ilipokea tathimini chanya kutoka kwa washiriki. Shukrani pia kwa ISP na IBG kwa msaada wao wa vifaa. Warsha ilidhaminiwa na VR SRL na kuandaliwa na Sanja Tibell (Systematic biology, IOB, UU) na Donatha Tibuhwa ( UDSM Tanzania).
Maelezo. Washiriki na wahadhiri kadhaa baada ya kuongozwa kwenda Linnaeus 'Hammarby siku ya mwisho ya warsha.
Washiriki na wasemaji wawili mbele ya mlango wa Old Zootis.
1. Ms. Zuhura Ndoika Mwanga
2. Mr. Juma Mahmud Hussein
3. Mr. Ibrahim Juma Vuga
4. Ms. Winnie Ernest Kimaro
5. Mr. Ferdinand Patrick Kisoka
6. Ms. Stella Gilbert Temu
7. Dr. Donatha Damian Tibuhwa
2016
Stella Gilbert Temu
Habari, Jina langu ni Stella Gilbert Temu, ni Mtanzania, nasoma Shahada ya Uzamivu ‘PhD’katika Chuo Kikuu cha Uppsala nchini Sweden. Chuo kina mazingira rafiki ya kujisomea na utafiti. Pia kina wanasayansi waliobobea kwenye fani mbalimbali ambao wamekuwa msaada mkubwa katika utafiti na masomo kwa ujumla. Nafanya utafiti kuhusu ‘Lichens’. Viumbe hawa wanapatikana kwa wingi duniani kote. Pia wana umuhimu katika maeneo mengi katika maisha ya wanadamu ikiwemo udhibiti wa mazingira, hivyo kuvutia utafiti zaidi kuhusu wao.
Malengo yangu baada ya kumaliza shule: Kutumia ujuzi nilioupata kuwasaidia wanasayansi hasa wadogo katika kukuza na kuendeleza utafiti zaidi kuhusu ‘lichens’ nchini Tanzania. Pia kuungana wanasayansi wa kimataifa katika utafiti wa ‘Lichens’.
Juma Hussein
Mimi ni Juma Hussein, mhadhiri msaidizi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Tanzanzia na pia ni mwanfunzi wa shahada ya Uzamivu (PhD) ya Biolojia utaratibu (Systematic Biology) katika chuo kikuu cha Uppsala, Uswidi (2016-2020). Nafanya utafiti unaohusiana na uyoga kutoka Tanzania. Tafiti hizi zinajikita kwanye uyoga vimelea ambao hushambulia miti na kuikausha kabisa hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao ya biashara kama korosho. Hivyo tunajifunza njia za uvamizi wa mimea hiyo na jinsi ya kuzuia maambukizi zaidi. Pia sehemu nyingine ya utafiti huo inahusisha uyoga unaotumiwa kama dawa na chakula.
Tafiti hizi zitakapokamilika zitasaidia kuongeza uelewa kuhusu uyoga vimilea na hivyokusaidia kutoa taarifa ya jinsi ya kupambana na vimelea hivyo. Halikadhalika, taarifa kuhusu virutubisho vinanyopatikana kwenye uyoga unaoliwa na utumikao kama dawa huenda zikasaidia kwenye ugunduzi wa dawa mbadala za kukabiliana na magonjwa hatari kama kisukari, kansa na kuongeza kinga ya mwili.